Kwa kuwa ufahamu juu ya maisha ya Peponi umezungukwa na hakika za kiimani, basi ulinganishi uliofanyika kitabuni humu unawianishwa na maisha halisi ya ulimwengu huu. Katika baadhi ya sura au sehemu, yametolewa maelezo linganishi ili kumuwezesha msomaji kupima na kutafakari ili kupata uoni huru unaotokana na hakika za kimsingi zenye hoja madhubuti. Kitabu hiki kimelenga kusaidia kumpa msomaji uhalisia wa kile ambacho pengine amekuwa akikisikia, kujifunza na kukiamini muda wote bila ya kuwa na walau taswira yake.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu aikubali jitihada hii, atusamehe upungufu wetu na atie Tawfiiq waja wake watakaokisoma waweze kuyafahamu vyema maudhui ya kitabu hiki. Maudhui haya yawe chachu ya kuwaweze kuishi kulingana na atakavyo YEYE, wapate kufaulu na kuzawadiwa Pepo tukufu.