Pamoja na wanasayansi kufanya jitihada kubwa za kitafiti kubaini ukubwa wake, mapana na umbali wake, ukubwa wa umbile la mbingu umepindukia uelewa wa Mwanaadamu licha ya kipawa kikubwa alichonacho cha akili yenye uwezo wa kutambuwa kila kitu. Mbingu hii na vilivyomo ndani yake vimetoka wapi? Vinaelekea wapi? Mwisho wake wapi? Na jinsi gani inavyofuata mtandao maalumu na wa pekee wa kutii sheria za kisayansi ambazo hazijulikani zilivyoanza?