logo
HARUN YAHYA
  • 1. Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo,
  • 2. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.
  • 3. Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.
  • 4. Na hakika wewe una tabia tukufu.
  • 5. Karibu utaona, na wao wataona,
  • 6. Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.
  • 7. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.
  • 8. Basi usiwat`ii wanao kadhibisha.
  • 9. Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.
  • 10. Wala usimt`ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,
  • 11. Mtapitapi, apitaye akifitini,
  • 12. Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,
  • 13. Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.
  • 14. Ati kwa kuwa ana mali na watoto!
  • 15. Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!
  • 16. Tutamtia kovu juu ya pua yake.
  • 17. Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi.
  • 18. Wala hawakusema: Mungu akipenda!
  • 19. Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!
  • 20. Likawa kama usiku wa giza.
  • 21. Asubuhi wakaitana.
  • 22. Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.
  • 23. Basi walikwenda na huku wakinong`onezana,
  • 24. Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
  • 25. Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.
  • 26. Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea!
  • 27. Bali tumenyimwa!
  • 28. Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?
  • 29. Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.
  • 30. Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.
  • 31. Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!
  • 32. Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
  • 33. Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua!
  • 34. Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.
  • 35. Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?
  • 36. Mna nini? Mnahukumu vipi?
  • 37. Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?
  • 38. Kuwa mtapata humo mnayo yapenda?
  • 39. Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia?
  • 40. Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya?
  • 41. Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.
  • 42. Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza,
  • 43. Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima -
  • 44. Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua.
  • 45. Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.
  • 46. Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?
  • 47. Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?
  • 48. Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa.
  • 49. Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.
  • 50. Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
  • 51. Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.
  • 52. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
SHIRIKI
logo
logo
logo
logo
logo
  • 1.Al-Fatihah
  • 2.Al Baqara
  • 3.Ali `Imran
  • 4.An-Nisa
  • 5.Al-Ma`idah
  • 6.Al-An`am
  • 7.Al-A`raf
  • 8.Al-Anfal
  • 9.At-Tawbah
  • 10.Yunus
  • 11.Hud
  • 12.Yusuf
  • 13.Ar-Ra`d
  • 14.Ibrahim
  • 15.Al-Hijr
  • 16.An-Nahl
  • 17.Al-Isra
  • 18.Al-Kahf
  • 19.Maryam
  • 20.Taha
  • 21.Al-Anbya
  • 22.Al-Haj
  • 23.Al-Mu`minun
  • 24.An-Nur
  • 25.Al-Furqan
  • 26.Ash-Shu`ara
  • 27.An-Naml
  • 28.Al-Qasas
  • 29.Al-`Ankabut
  • 30.Ar-Rum
  • 31.Luqman
  • 32.As-Sajdah
  • 33.Al-Ahzab
  • 34.Saba
  • 35.Faatir
  • 36.Ya-Sin
  • 37.As-Saffat
  • 38.Sad
  • 39.Az-Zumar
  • 40.Ghafir
  • 41.Fussilat
  • 42.sh-Shuraa
  • 43.Az-Zukhruf
  • 44.Ad-Dukhan
  • 45.Al-Jathiyah
  • 46.Al-Ahqaf
  • 47.Muhammad
  • 48.Al-Fath
  • 49.Al-Hujurat
  • 50.Qaf
  • 51.Adh-Dhariyat
  • 52.At-Tur
  • 53.An-Najm
  • 54.Al-Qamar
  • 55.Ar-Rahman
  • 56.Al-Waqi`ah
  • 57.Al-Hadid
  • 58.Al-Mujadila
  • 59.Al-Hashr
  • 60.Al-Mumtahanah
  • 61.As-Saf
  • 62.Al-Jumu`ah
  • 63.Al-Munafiqun
  • 64.At-Taghabun
  • 65.At-Talaq
  • 66.At-Tahrim
  • 67.Al-Mulk
  • 68.Al-Qalam
  • 69.Al-Haqqah
  • 70.Al-Ma`arij
  • 71.Nuh
  • 72.Al-Jinn
  • 73.Al-Muzzammil
  • 74.Al-Muddaththir
  • 75.Al-Qiyamah
  • 76.Al-Insan
  • 77.Al-Mursalat
  • 78.An-Naba
  • 79.An-Nazi`at
  • 80.Abasa
  • 81.At-Takwir
  • 82.Al-Infitar
  • 83.Al-Mutaffifin
  • 84.Al-Inshiqaq
  • 85.Al-Buruj
  • 86.At-Tariq
  • 87.Al-A`la
  • 88.Al-Ghashiyah
  • 89.Al-Fajr
  • 90.Al-Balad
  • 91.Ash-Shams
  • 92.Al-Layl
  • 93.Ad-Duhaa
  • 94.Ash-Sharh
  • 95.At-Tin
  • 96.Al-`Alaq
  • 97.Al-Qadr
  • 98.Al-Bayyinah
  • 99.Az-Zalzalah
  • 100.Al-`Adiyat
  • 101.Al-Qari`ah
  • 102.At-Takathur
  • 103.Al-`Asr
  • 104.Al-Humazah
  • 105.Al-Fil
  • 106.Quraysh
  • 107.Al-Ma`un
  • 108.Al-Kawthar
  • 109.Al-Kafirun
  • 110.An-Nasr
  • 111.Al-Masad
  • 112.Al-Ikhlas
  • 113.Al-Falaq
  • 114.An-Nas