logo
HARUN YAHYA
  • 1. Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
  • 2. Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
  • 3. Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.
  • 4. Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
  • 5. Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
  • 6. Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha;
  • 7. Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,
  • 8. Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
  • 9. Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
  • 10. Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!
  • 11. Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
  • 12. Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.
  • 13. Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
  • 14. Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
  • 15. Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?
  • 16. Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
  • 17. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?
  • 18. Kina A`di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
  • 19. Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
  • 20. Ukiwang`oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng`olewa.
  • 21. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
  • 22. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?
  • 23. Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
  • 24. Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
  • 25. Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
  • 26. Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
  • 27. Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.
  • 28. Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.
  • 29. Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
  • 30. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
  • 31. Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.
  • 32. Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur`ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
  • 33. Kaumu Lut`i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
  • 34. Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut`i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
  • 35. Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
  • 36. Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.
  • 37. Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
  • 38. Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
  • 39. Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!
  • 40. Na hakika tumeisahilisha Qur`ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
  • 41. Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
  • 42. Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
  • 43. Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
  • 44. Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
  • 45. Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
  • 46. Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.
  • 47. Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
  • 48. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!
  • 49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
  • 50. Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
  • 51. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
  • 52. Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
  • 53. Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
  • 54. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
  • 55. Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
SHIRIKI
logo
logo
logo
logo
logo
  • 1.Al-Fatihah
  • 2.Al Baqara
  • 3.Ali `Imran
  • 4.An-Nisa
  • 5.Al-Ma`idah
  • 6.Al-An`am
  • 7.Al-A`raf
  • 8.Al-Anfal
  • 9.At-Tawbah
  • 10.Yunus
  • 11.Hud
  • 12.Yusuf
  • 13.Ar-Ra`d
  • 14.Ibrahim
  • 15.Al-Hijr
  • 16.An-Nahl
  • 17.Al-Isra
  • 18.Al-Kahf
  • 19.Maryam
  • 20.Taha
  • 21.Al-Anbya
  • 22.Al-Haj
  • 23.Al-Mu`minun
  • 24.An-Nur
  • 25.Al-Furqan
  • 26.Ash-Shu`ara
  • 27.An-Naml
  • 28.Al-Qasas
  • 29.Al-`Ankabut
  • 30.Ar-Rum
  • 31.Luqman
  • 32.As-Sajdah
  • 33.Al-Ahzab
  • 34.Saba
  • 35.Faatir
  • 36.Ya-Sin
  • 37.As-Saffat
  • 38.Sad
  • 39.Az-Zumar
  • 40.Ghafir
  • 41.Fussilat
  • 42.sh-Shuraa
  • 43.Az-Zukhruf
  • 44.Ad-Dukhan
  • 45.Al-Jathiyah
  • 46.Al-Ahqaf
  • 47.Muhammad
  • 48.Al-Fath
  • 49.Al-Hujurat
  • 50.Qaf
  • 51.Adh-Dhariyat
  • 52.At-Tur
  • 53.An-Najm
  • 54.Al-Qamar
  • 55.Ar-Rahman
  • 56.Al-Waqi`ah
  • 57.Al-Hadid
  • 58.Al-Mujadila
  • 59.Al-Hashr
  • 60.Al-Mumtahanah
  • 61.As-Saf
  • 62.Al-Jumu`ah
  • 63.Al-Munafiqun
  • 64.At-Taghabun
  • 65.At-Talaq
  • 66.At-Tahrim
  • 67.Al-Mulk
  • 68.Al-Qalam
  • 69.Al-Haqqah
  • 70.Al-Ma`arij
  • 71.Nuh
  • 72.Al-Jinn
  • 73.Al-Muzzammil
  • 74.Al-Muddaththir
  • 75.Al-Qiyamah
  • 76.Al-Insan
  • 77.Al-Mursalat
  • 78.An-Naba
  • 79.An-Nazi`at
  • 80.Abasa
  • 81.At-Takwir
  • 82.Al-Infitar
  • 83.Al-Mutaffifin
  • 84.Al-Inshiqaq
  • 85.Al-Buruj
  • 86.At-Tariq
  • 87.Al-A`la
  • 88.Al-Ghashiyah
  • 89.Al-Fajr
  • 90.Al-Balad
  • 91.Ash-Shams
  • 92.Al-Layl
  • 93.Ad-Duhaa
  • 94.Ash-Sharh
  • 95.At-Tin
  • 96.Al-`Alaq
  • 97.Al-Qadr
  • 98.Al-Bayyinah
  • 99.Az-Zalzalah
  • 100.Al-`Adiyat
  • 101.Al-Qari`ah
  • 102.At-Takathur
  • 103.Al-`Asr
  • 104.Al-Humazah
  • 105.Al-Fil
  • 106.Quraysh
  • 107.Al-Ma`un
  • 108.Al-Kawthar
  • 109.Al-Kafirun
  • 110.An-Nasr
  • 111.Al-Masad
  • 112.Al-Ikhlas
  • 113.Al-Falaq
  • 114.An-Nas