logo
HARUN YAHYA
  • 1. H`a Mim
  • 2. Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha,
  • 3. Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
  • 4. Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima,
  • 5. Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
  • 6. Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
  • 7. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
  • 8. Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
  • 9. Lakini wao wanacheza katika shaka.
  • 10. Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapo leta moshi ulio dhaahiri,
  • 11. Utakao wafunika watu: Hii ni adhabu chungu!
  • 12. Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
  • 13. Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
  • 14. Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.
  • 15. Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
  • 16. Siku tutayo yashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
  • 17. Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
  • 18. Akasema: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
  • 19. Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
  • 20. Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
  • 21. Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.
  • 22. Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: Hakika watu hawa ni wakosefu.
  • 23. Mwenyezi Mungu akasema: Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
  • 24. Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao hao ni jeshi litakalo zamishwa.
  • 25. Mabustani mangapi, na chemchem ngapi waliziacha!
  • 26. Na mimea na vyeo vitukufu!
  • 27. Na neema walizo kuwa wakijistareheshea!
  • 28. Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wenginewe.
  • 29. La mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
  • 30. Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
  • 31. Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
  • 32. Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wenginewe.
  • 33. Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
  • 34. Hakika hawa wanasema:
  • 35. Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
  • 36. Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
  • 37. Je! Ni wao bora au watu wa Tubbaa` na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
  • 38. Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake kwa mchezo.
  • 39. Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
  • 40. Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
  • 41. Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
  • 42. Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
  • 43. Hakika Mti wa Zaqqum,
  • 44. Ni chakula cha mwenye dhambi.
  • 45. Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
  • 46. Kama kutokota kwa maji ya moto.
  • 47. (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
  • 48. Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
  • 49. Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
  • 50. Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
  • 51. Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,
  • 52. Katika mabustani na chemchem,
  • 53. Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,
  • 54. Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.
  • 55. Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
  • 56. Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
  • 57. Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
  • 58. Basi tumeifanya nyepesi hii Qur`ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
  • 59. Ngoja tu, na wao wangoje pia.
SHIRIKI
logo
logo
logo
logo
logo
  • 1.Al-Fatihah
  • 2.Al Baqara
  • 3.Ali `Imran
  • 4.An-Nisa
  • 5.Al-Ma`idah
  • 6.Al-An`am
  • 7.Al-A`raf
  • 8.Al-Anfal
  • 9.At-Tawbah
  • 10.Yunus
  • 11.Hud
  • 12.Yusuf
  • 13.Ar-Ra`d
  • 14.Ibrahim
  • 15.Al-Hijr
  • 16.An-Nahl
  • 17.Al-Isra
  • 18.Al-Kahf
  • 19.Maryam
  • 20.Taha
  • 21.Al-Anbya
  • 22.Al-Haj
  • 23.Al-Mu`minun
  • 24.An-Nur
  • 25.Al-Furqan
  • 26.Ash-Shu`ara
  • 27.An-Naml
  • 28.Al-Qasas
  • 29.Al-`Ankabut
  • 30.Ar-Rum
  • 31.Luqman
  • 32.As-Sajdah
  • 33.Al-Ahzab
  • 34.Saba
  • 35.Faatir
  • 36.Ya-Sin
  • 37.As-Saffat
  • 38.Sad
  • 39.Az-Zumar
  • 40.Ghafir
  • 41.Fussilat
  • 42.sh-Shuraa
  • 43.Az-Zukhruf
  • 44.Ad-Dukhan
  • 45.Al-Jathiyah
  • 46.Al-Ahqaf
  • 47.Muhammad
  • 48.Al-Fath
  • 49.Al-Hujurat
  • 50.Qaf
  • 51.Adh-Dhariyat
  • 52.At-Tur
  • 53.An-Najm
  • 54.Al-Qamar
  • 55.Ar-Rahman
  • 56.Al-Waqi`ah
  • 57.Al-Hadid
  • 58.Al-Mujadila
  • 59.Al-Hashr
  • 60.Al-Mumtahanah
  • 61.As-Saf
  • 62.Al-Jumu`ah
  • 63.Al-Munafiqun
  • 64.At-Taghabun
  • 65.At-Talaq
  • 66.At-Tahrim
  • 67.Al-Mulk
  • 68.Al-Qalam
  • 69.Al-Haqqah
  • 70.Al-Ma`arij
  • 71.Nuh
  • 72.Al-Jinn
  • 73.Al-Muzzammil
  • 74.Al-Muddaththir
  • 75.Al-Qiyamah
  • 76.Al-Insan
  • 77.Al-Mursalat
  • 78.An-Naba
  • 79.An-Nazi`at
  • 80.Abasa
  • 81.At-Takwir
  • 82.Al-Infitar
  • 83.Al-Mutaffifin
  • 84.Al-Inshiqaq
  • 85.Al-Buruj
  • 86.At-Tariq
  • 87.Al-A`la
  • 88.Al-Ghashiyah
  • 89.Al-Fajr
  • 90.Al-Balad
  • 91.Ash-Shams
  • 92.Al-Layl
  • 93.Ad-Duhaa
  • 94.Ash-Sharh
  • 95.At-Tin
  • 96.Al-`Alaq
  • 97.Al-Qadr
  • 98.Al-Bayyinah
  • 99.Az-Zalzalah
  • 100.Al-`Adiyat
  • 101.Al-Qari`ah
  • 102.At-Takathur
  • 103.Al-`Asr
  • 104.Al-Humazah
  • 105.Al-Fil
  • 106.Quraysh
  • 107.Al-Ma`un
  • 108.Al-Kawthar
  • 109.Al-Kafirun
  • 110.An-Nasr
  • 111.Al-Masad
  • 112.Al-Ikhlas
  • 113.Al-Falaq
  • 114.An-Nas