logo
HARUN YAHYA
  • 1. Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
  • 2. Na kwa wenye kukataza mabaya.
  • 3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
  • 4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
  • 5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
  • 6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
  • 7. Na kulinda na kila shet`ani a`si.
  • 8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.
  • 9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
  • 10. Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng`ara.
  • 11. Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
  • 12. Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
  • 13. Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
  • 14. Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
  • 15. Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
  • 16. Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
  • 17. Hata baba zetu wa zamani?
  • 18. Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
  • 19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
  • 20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
  • 21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
  • 22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu -
  • 23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
  • 24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
  • 25. Mna nini? Mbona hamsaidiani?
  • 26. Bali hii leo, watasalimu amri.
  • 27. Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
  • 28. Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.
  • 29. Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
  • 30. Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
  • 31. Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.
  • 32. Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
  • 33. Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.
  • 34. Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
  • 35. Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa `Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
  • 36. Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?
  • 37. Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.
  • 38. Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
  • 39. Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
  • 40. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
  • 41. Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
  • 42. Matunda, nao watahishimiwa.
  • 43. Katika Bustani za neema.
  • 44. Wako juu ya viti wamekabiliana.
  • 45. Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
  • 46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
  • 47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.
  • 48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.
  • 49. Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
  • 50. Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
  • 51. Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki
  • 52. Aliye kuwa akinambia: Hivyo wewe ni katika wanao sadiki
  • 53. Ati tukisha kufa tukawa udongo na mafupa, ndio tutalipwa na kuhisabiwa?
  • 54. Atasema: Je! Nyie mnawaona?
  • 55. Basi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.
  • 56. Atasema: Wallahi! Ulikaribia kunipoteza.
  • 57. Na lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi bila ya shaka ningeli kuwa miongoni mwa walio hudhurishwa.
  • 58. Je! Sisi hatutakufa,
  • 59. Isipo kuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.
  • 60. Hakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.
  • 61. Kwa mfano wa haya nawatende watendao.
  • 62. Je! Kukaribishwa hivi si ndio bora, au mti wa Zaqqum?
  • 63. Hakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa walio dhulumu.
  • 64. Hakika huo ni mti unao toka katikati ya Jahannamu.
  • 65. Mashada ya matunda yake kama kwamba vichwa vya mashet`ani.
  • 66. Basi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo.
  • 67. Kisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji yamoto yaliyo chemka.
  • 68. Kisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa kwenye Jahannamu.
  • 69. Hakika waliwakuta baba zao wamepotea.
  • 70. Na wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.
  • 71. Na bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.
  • 72. Na Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.
  • 73. Basi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walio onywa.
  • 74. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
  • 75. Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.
  • 76. Na tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.
  • 77. Na tuliwajaalia dhuriya zake ndio wenye kubakia.
  • 78. Na tukamwachia (sifa njema) kwa walio kuja baadaye.
  • 79. Iwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!
  • 80. Kwa hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
  • 81. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
  • 82. Kisha tukawazamisha wale wengine.
  • 83. Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake,
  • 84. Alipo mjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.
  • 85. Alimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?
  • 86. Kwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?
  • 87. Mnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?
  • 88. Kisha akapiga jicho kutazama nyota.
  • 89. Akasema: Hakika mimi ni mgonjwa!
  • 90. Nao wakamwacha, wakampa kisogo.
  • 91. Basi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?
  • 92. Mna nini hata hamsemi?
  • 93. Kisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.
  • 94. Basi wakamjia upesi upesi.
  • 95. Akasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyo vichonga wenyewe?
  • 96. Na hali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni nyinyi na hivyo mnavyo vifanya!
  • 97. Wakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!
  • 98. Basi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini.
  • 99. Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.
  • 100. Ewe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.
  • 101. Basi tukambashiria mwana aliye mpole.
  • 102. Basi alipo fika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri.
  • 103. Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
  • 104. Tulimwita: Ewe Ibrahim!
  • 105. Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.
  • 106. Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
  • 107. Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.
  • 108. Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.
  • 109. Iwe salama kwa Ibrahim!
  • 110. Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
  • 111. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
  • 112. Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.
  • 113. Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.
  • 114. Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
  • 115. Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.
  • 116. Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.
  • 117. Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.
  • 118. Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
  • 119. Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye.
  • 120. Iwe salama kwa Musa na Haruni!
  • 121. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
  • 122. Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.
  • 123. Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
  • 124. Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?
  • 125. Mnamwomba Baa`li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
  • 126. Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?
  • 127. Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
  • 128. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
  • 129. Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.
  • 130. Iwe salama kwa Ilyas.
  • 131. Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
  • 132. Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
  • 133. Na hakika Lut`i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
  • 134. Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,
  • 135. Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.
  • 136. Kisha tukawaangamiza wale wengineo.
  • 137. Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
  • 138. Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
  • 139. Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
  • 140. Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
  • 141. Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.
  • 142. Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
  • 143. Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
  • 144. Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
  • 145. Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
  • 146. Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung`unye.
  • 147. Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
  • 148. Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
  • 149. Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?
  • 150. Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
  • 151. Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
  • 152. Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
  • 153. Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
  • 154. Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
  • 155. Hamkumbuki?
  • 156. Au mnayo hoja iliyo wazi?
  • 157. Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
  • 158. Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
  • 159. Subhana `Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.
  • 160. Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
  • 161. Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
  • 162. Hamwezi kuwapoteza
  • 163. Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
  • 164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.
  • 165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
  • 166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
  • 167. Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
  • 168. Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
  • 169. Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.
  • 170. Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
  • 171. Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.
  • 172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
  • 173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
  • 174. Basi waachilie mbali kwa muda.
  • 175. Na watazame, nao wataona.
  • 176. Je! Wanaihimiza adhabu yetu?
  • 177. Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.
  • 178. Na waache kwa muda.
  • 179. Na tazama, na wao wataona.
  • 180. Subhana Rabbi`l`Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia.
  • 181. Na Salamu juu ya Mitume.
  • 182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
SHIRIKI
logo
logo
logo
logo
logo
  • 1.Al-Fatihah
  • 2.Al Baqara
  • 3.Ali `Imran
  • 4.An-Nisa
  • 5.Al-Ma`idah
  • 6.Al-An`am
  • 7.Al-A`raf
  • 8.Al-Anfal
  • 9.At-Tawbah
  • 10.Yunus
  • 11.Hud
  • 12.Yusuf
  • 13.Ar-Ra`d
  • 14.Ibrahim
  • 15.Al-Hijr
  • 16.An-Nahl
  • 17.Al-Isra
  • 18.Al-Kahf
  • 19.Maryam
  • 20.Taha
  • 21.Al-Anbya
  • 22.Al-Haj
  • 23.Al-Mu`minun
  • 24.An-Nur
  • 25.Al-Furqan
  • 26.Ash-Shu`ara
  • 27.An-Naml
  • 28.Al-Qasas
  • 29.Al-`Ankabut
  • 30.Ar-Rum
  • 31.Luqman
  • 32.As-Sajdah
  • 33.Al-Ahzab
  • 34.Saba
  • 35.Faatir
  • 36.Ya-Sin
  • 37.As-Saffat
  • 38.Sad
  • 39.Az-Zumar
  • 40.Ghafir
  • 41.Fussilat
  • 42.sh-Shuraa
  • 43.Az-Zukhruf
  • 44.Ad-Dukhan
  • 45.Al-Jathiyah
  • 46.Al-Ahqaf
  • 47.Muhammad
  • 48.Al-Fath
  • 49.Al-Hujurat
  • 50.Qaf
  • 51.Adh-Dhariyat
  • 52.At-Tur
  • 53.An-Najm
  • 54.Al-Qamar
  • 55.Ar-Rahman
  • 56.Al-Waqi`ah
  • 57.Al-Hadid
  • 58.Al-Mujadila
  • 59.Al-Hashr
  • 60.Al-Mumtahanah
  • 61.As-Saf
  • 62.Al-Jumu`ah
  • 63.Al-Munafiqun
  • 64.At-Taghabun
  • 65.At-Talaq
  • 66.At-Tahrim
  • 67.Al-Mulk
  • 68.Al-Qalam
  • 69.Al-Haqqah
  • 70.Al-Ma`arij
  • 71.Nuh
  • 72.Al-Jinn
  • 73.Al-Muzzammil
  • 74.Al-Muddaththir
  • 75.Al-Qiyamah
  • 76.Al-Insan
  • 77.Al-Mursalat
  • 78.An-Naba
  • 79.An-Nazi`at
  • 80.Abasa
  • 81.At-Takwir
  • 82.Al-Infitar
  • 83.Al-Mutaffifin
  • 84.Al-Inshiqaq
  • 85.Al-Buruj
  • 86.At-Tariq
  • 87.Al-A`la
  • 88.Al-Ghashiyah
  • 89.Al-Fajr
  • 90.Al-Balad
  • 91.Ash-Shams
  • 92.Al-Layl
  • 93.Ad-Duhaa
  • 94.Ash-Sharh
  • 95.At-Tin
  • 96.Al-`Alaq
  • 97.Al-Qadr
  • 98.Al-Bayyinah
  • 99.Az-Zalzalah
  • 100.Al-`Adiyat
  • 101.Al-Qari`ah
  • 102.At-Takathur
  • 103.Al-`Asr
  • 104.Al-Humazah
  • 105.Al-Fil
  • 106.Quraysh
  • 107.Al-Ma`un
  • 108.Al-Kawthar
  • 109.Al-Kafirun
  • 110.An-Nasr
  • 111.Al-Masad
  • 112.Al-Ikhlas
  • 113.Al-Falaq
  • 114.An-Nas