1. Ole wake kila safihi, msengenyaji!
2. Aliye kusanya mali na kuyahisabu.
3. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele!
4. Hasha! Atavurumishwa katika H`ut`ama.
5. Na nani atakujuvya ni nini H`ut`ama?
6. Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa.
7. Ambao unapanda nyoyoni.
8. Hakika huo utafungiwa nao
9. Kwenye nguzo zilio nyooshwa.